Marekani yailaumu Rwanda kwa kuhatarisha usalama
13 Desemba 2025
Matangazo
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Mike Waltz, jana Ijumaa aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba badala ya kupiga hatua kuelekea amani kama walivyoona chini ya uongozi wa Rais Donald Trump katika wiki za hivi karibuni, Rwanda inaongoza eneo hilo kuelekea ukosefu wa utulivu na vita.
Pia amesema Marekani ina wasiwasi mkubwa na inazidi kukatishwa tamaa kwa kuzuka upya kwa ghasia.
Waltz ameongeza kuwa vikosi vya ulinzi vya Rwanda vimetoa msaada wa vifaa, mipangilio na mafunzo kwa M23 pamoja na kuisadia vitani nchini Kongo kwa kupeleka takriban wanajeshi 5,000 hadi 7,000, bila kujumuisha uwezekano wa nyongeza ya idadi hiyo wakati wa mashambulizi ya hivi karibuni.