Marekani yaiondolea Belarus baadhi ya vikwazo vya kibiashara
13 Desemba 2025
Matangazo
John Coale, mjumbe maalum wa Marekani kwa Belarus, alitangaza hilo baada ya kukutana na kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko mjini Minsk jana na leo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Coale aliyataja mazungumzo ya siku hiyo mbili kuwa yenye tija.
Mjumbe huyo wa Marekani amesema kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya Washington na
Minsk lilikuwa lengo lao.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Belarus Belta, Coale amesema wanaondoa vikwazo, wanawaaachilia wafungwa, wanaendelea na mazungumzo na kwamba uhusiano kati ya nchi hizo ulikuwa unatoka kuwa mchanga hadi kwa hatua ya kujiamini zaidi.
Kwa upande wake Rais Lukashenko amewasamehe wafungwa 123 kwa kubadilshana na na kuondolewa kwa vikwazo hivyo vya Marekani.