1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaipunguzia fedha za dhamana Israel:

26 Novemba 2003
WASHINGTON: Serikali ya Marekani itapunguza karibu dollar millioni 300 katika mkusanyiko wa dollar billioni kadhaa za kudhamini mikopo inayotaka kukopa Israel. Kupunguzwa fedha hizo kunatokana na harakati za kujenga makaazi ya wayahudi katika maeneo inayoyakalia ya Wapalastina na ujenzi wa ukuta katika Ukingo wa Magharibi. Israel inatoa hoja kuwa ukuta huo ni kuepusha mashambulio ya kigaidi ya Wapalastina washupavu. Na chama kikuu cha upinzani nchini Israel ‚LABOUR PARTY, kimechapisha mpango wake wa amani, na unatazamia kuundwa dola ya Wapalastina, na Israel irudi kwenye mipaka ya mwaka 1967, isipokuwa kutokana na sababu za usalama.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW