1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaisaidia Haiti kwa uchunguzi

13 Julai 2021

Marekani imesema inaisaidia Haiti kufanya uchunguzi kuhusu mauwaji ya rais Jovenel Moise na haijaondoa uwezekano wa kutuma wanajeshi wake baada ya ombi kutolewa na serikali mjini Port-au-Prince.

Haiti | Ermordung Präsident Jovenel Moise
Picha: Valerie AFP/Getty Images

Taarifa kutoka kwa wizara ya sheria ya Marekani, imesema Washington inaisaidia polisi ya Haiti katika uchunguzi wa kifo cha rais Moise kwa kushirikiana na wadau wengine. Soma Haiti: Serikali ya mpito yaomba wanajeshi kutoka Marekani, Umoja wa Mataifa

Maafisa wakuu wa Marekani wamefanya tathmini ya awali nchini Haiti na wizara hiyo itaendelea kuunga mkono serikali ya Haiti katika kukagua ukweli na mazingira yanayozunguka shambulizi hilo baya. soma zaidiRaia wa Haiti akamatwa akihusishwa na mauaji ya Rais Moise

Taarifa ya Marekani imeongeza kuwa itafanya uchunguzi zaidi kubaini iwapo sheria za Marekani zilikiukwa.

Wanasiasa lazima waungane

Mkuu wa polisi Haiti Léon CharlesPicha: AFP via Getty Images

Akizungumza na wanahabari rais wa Marekani Joe Biden amesema wanasiasa lazima waungane, na kuwa Marekani iko tayari kutoa msaada wake.

Wakati huo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Anthony Blinken amesema "Tunawasihi viongozi wa kisiasa kuileta nchi pamoja katika maono ya umoja, amani na usalama na kuweka misingi bora kuelekea uchaguzi huru na wa haki mwaka huu. Jana, tulituma ujumbe Port au Prince kutathmini hali hiyo, ambapo, pamoja na mawasiliano yetu ya mara kwa mara na maafisa wa Haiti na washikadau wengine, itasaidia kujua ni jinsi gani Marekani inaweza kusaidia Haiti katika wakati huu mgumu."

Nia ya mauwaji haijabainika

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jen PsakiPicha: Evan Vucci/AP/dpa/picture alliance

Msemaji wa Ikulu ya Marekani  Jen Psaki amesema maafisa wa serikali na  usalama wa nchi hiyo waliotembelea Haiti siku ya Jumapili wamebaini ukosefu wa utulivu baada ya mauaji ya Moise.

Ujumbe wa Marekani unaowakilisha wizara za sheria, usalama wa ndani, mambo ya kigeni na Baraza la Taifa la Usalama  ulikutana na maafisa wakuu wa Haiti. Soma Mustakabali wa Haiti mashakani baada ya mauaji ya rais

Psaki ameongeza kuwa ni wazi kwamba hakuna kilicho wazi kuhusu hatma ya uongozi wa kisiasa wa nchi hiyo katika siku zijazo.

Hadi sasa nia ya mauwaji ya rais Moise haijabainika na maswali yanaendelea kuzunguka juu ya nani aliyepanga mauaji hayo.

Msemaji wa baraza la Usalama la Marekani Emily Horne amesema ujumbe huo ulihakiki miundombinu muhimu ya usalama na walikutana na maafisa wa serikali ya Haiti pamoja na polisi ambao wanaongoza uchunguzi wa mauaji hayo. Soma Raia wa Marekani na Colombia washukiwa kuhusika na mauaji ya rais wa Haiti

Horne ameongeza kuwa walikutana pia na viongozi wa kisiasa wa Haiti, akiwemo waziri mkuu wa mpito Claude Joseph na rais wa bunge la seneti Joseph Lambert ili  kuhamasisha mazungumzo ya wazi na yenye tija kufikia makubaliano ya kisiasa ambayo yanaweza kuiwezesha nchi kufanya uchaguzi huru na wa haki.

 

/AFP

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW