1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Marekani yaisamehe Somalia deni la zaidi ya dola bilioni 1

6 Novemba 2024

Marekani imefutilia mbali deni la zaidi ya dola bilioni 1 inayozidai Somalia. Makubaliano hayo yalitiwa saini na waziri wa fedha wa Somalia Bihi Egeh na balozi wa Marekani, Somalia Richard Riley.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akizungumza na waandishi wa habari katika kikao cha 37 cha Baraza Kuu la Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia mnamo Februari 17,2024
Rais wa Somalia Hassan Sheikh MohamudPicha: REUTERS

Wakati wa hafla ya kutia saini makubaliano hayo ya pande mbili, Riley alisema kuwa msamaha huo ni sehemu kubwa zaidi ya deni jumla la dola bilioni 4.5 inazodaiwa Somaliana nchi nyingi ambalo lilisamehewa chini ya makubaliano na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia mwezi Desemba.

Egeh aishukuru Marekani kwa msaada wake kwa Somalia

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, Egeh aliishukuru Marekani kwa msaada wake usioyumba wa mageuzi ya kiuchumi na ukuaji nchini Somalia.

Marekani yajieleza kuwa mshirika thabiti kwa watu wa Somalia

Ubalozi wa Marekani umesema msamaha huo wa deni ni mbali na dola bilioni 1.2 za misaada ya kimaendeleo, kiuchumi, kiusalama na ya kibinadamu ambayo Marekani imetoa kwaSomalia mwaka huu, ikiielezea Marekani kama mshirika thabiti kwa watu wa Somalia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW