SiasaUrusi
Marekani yaishtumu Urusi kwa kutishia wafanyikazi wake
29 Agosti 2023Matangazo
Mfanyikazi huyo wa ubalozi anashutumiwa kwa kukusanya taarifa juu ya vita vya nchini Ukraine kwa niaba ya Marekani.
Shirika la habari la serikali ya Urusi TASS imeinukuu idara ya usalama ya Urusi FSB kuwa, Robert Shonov, raia wa Urusi aliwasilisha taarifa kwa wafanyikazi wa ubalozi wa Marekanimjini Moscow juu ya kampeni ya kuandikisha vijana kujiunga na jeshi nchini Urusi.
FSB imesema inapanga kuwahoji wafanyikazi wa ubalozi wa Marekani waliokuwa wakiwasiliana na Shonov, ambaye tayari amekamatwa tangu mwezi Mei.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Mathew Miller ameeleza kuwa, tuhuma dhidi ya Shonov, ambaye Marekani inasema aliajiriwa na kampuni iliyopewa kandarasi kwenye ubalozi wake, hazina ukweli wowote.