Marekani yaitaka ADC iishinikize ZImbabwe
18 Agosti 2007Lusaka /Washington:
Marekani imewatolea mwito viongozi wa kusini mwa Afrika wazidishe shinikizo ili kumaliza mzozo nchini Zimbabwe.Mwito huo umetolewa muda mfupi baada ya kumalizika mkutano wa kilele wa jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC mjini Lusaka Zambia.”Tunawahimiza viongozi wa SADC wazidishe juhudi za kuupatia ufumbuzi wa kudumu mzozo wa Zimbabwe” amesema hayo msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani Sean McCormack.”Wananchi wa Zimbabwe wanastahiki hali bora.”Ameongeza kusema.Msemaji huyo wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani ameukosoa utawala wa rais Robert Mugabe kwa kuwakandamiza wakuu wa mashirika ya huduma za jamii,,ikiwa ni pamoja na mashirika ya kidini,wafanya biashara na vyama vya kisiasa.Mwenyekiti mpya wa jumuia hiyo ya maendeleo kusini mwa Afrika,rais Levy Mwanawasa wa Zambia,ameuambia mkutano wa waandishi habari mwisho mwa mkutano wa kjilele wa SADC tunanukuu:Mzozo wa Zimbabwe unatiwa chunvi.”