1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaitaka Mali kuwawajibisha waliofanya mauaji Moura

16 Mei 2023

Marekani imewatolea wito viongozi wa kijeshi wa Mali kuanzisha uchunguzi huru na wa haki kuwawajibisha wale wote waliohusika na mauaji ya watu wapatao 500 wakati wa operesheni ya mwaka jana katika kijiji cha Moura.

Mali | Colonel Assimi Goita
Picha: Malik Konate/AFP

Hayo yanajiri baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kubaini kuwa utawala wa kijeshi nchini Mali ulihusika katika mauaji hayo huku Washington ikiwatuhumu mamluki wa Urusi wa Wagner wanaoungwa mkono na Ikulu ya Kremlin.

Umoja wa Mataifa wataka kuchunguza mauwaji ya Mali

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani Matthew Miller amesema nchi yake inasikitishwa na vitendo vya kutojali maisha ya binaadamu vilivyoendeshwa huko Moura na wanajeshi wa Mali wakishirikiana na mamluki hao wa Wagner aliyowaita shirika la uhalifu la kimataifa.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW