1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Marekani yaiwekea vikwazo Rwanda kwa kuwaunga mkono M23

3 Machi 2026

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Jeshi la Rwanda na maafisa wake wanne waandamizi inaowatuhumu kuliunga mkono kundi la M23 linalohusishwa na matendo ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu mashariki mwa Kongo.

Marekani Washington D.C. 2025 | Donald Trump akiwa na viongozi wa Rwanda na Kongo
Mkataba wa amani kati ya Marais Felix Tshisekedi wa Kongo na Paul Kagame wa Rwanda ulitiwa saini mbele ya Rais Donald Trump wa Marekani mjini Washington Disemba mwaka 2025.Picha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP

Tangazo la vikwazo hivyo limetolewa jana jioni na Wizara ya Fedha ya Marekani ambayo imedai kwamba bila msaada wa serikali na jeshi la Rwanda, kundi la M23 lisingeweza kufanya mashambulizi nchini Kongo.  Kwa miaka mingi sasa inaaminika kuwa Rwanda ndiye mfadhili mkuu wa kundi la M23

Miongoni mwa waliowekewa vikwazo ni Mkuu wa Jeshi la Rwanda, Jenerali Mubarakh Muganga, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Vincent Nyakarundi na makamanda wengine wawili wa ngazi ya juu.

Utawala wa Rais Donald Trump umekasirishwa na kuendelea kwa mashambulizi ya kundi la M23 licha ya kutiwa saini kwa makubaliano ya amani kati ya Marais Felix Tshisekedi wa Kongo na Paul Kagame wa Rwanda mjini Washington Disemba mwaka jana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW