Marekani yaiwekea vikwazo Syria:
13 Desemba 2003Matangazo
WASHINGTON: Rais wa Marekani George W. Bush amesaini sheria ya kuwekewa vikwazo Syria. Vikwazo hivyo vya kiuchumi na kidiplomasia vimekusudiwa kuifanya Syria iache kile ambacho Marekani inashutumu ni kuunga mkono makundi ya kigaidi, iache kuunda silaha za kuangamiza pamoja na kuhamisha wanajeshi wake kutoka Libanon. Hii leo wabunge wanane wa Kimarekani waliwasili Damascus kuzungumza na serikali ya Syria kuhusu shutuma za Marekani kwamba Syria inawaachilia wapiganaji wa kigeni kutumia ardhi yake kuingilia Iraq na kuwaunga mkono wafuasi wa Rais aliyepinduliwa wa Iraq, Saddam Hussein.
