1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaiwekea vikwazo vikubwa sekta ya mafuta ya Urusi

23 Oktoba 2025

Marekani imetangaza vikwazo vipya vikubwa kwa sekta ya mafuta ya Urusi.

Rais Donald Trump akiwa na Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte
Rais Donald Trump akiwa na Katibu Mkuu wa NATO Mark RuttePicha: Aaron Schwartz/abaca/picture alliance

Vikwazo hivyo vinavyolenga kumpelekea Rais Vladimir Putin kukubali kufanya mazungumzo ya amani na hatimaye kuvimaliza vita nchini Ukraine.

Vikwazo hivyo dhidi ya kampuni kubwa za mafuta za Rosneft na Lukoil vinafuatia miezi kadhaa ya miito kutoka kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ya kumtaka Trump aiwekee urusi vikwazo vikubwa zaidi katika sekta ya mafuta ya nchi hiyo.

Sekta hiyo ya mafuta ni muhimu katika kuendesha uchumi wa Urusi na imeuwezesha utawala wa Putin kuendelea na vita dhidi ya Ukraine licha ya kutengwa pakubwa kimataifa.

Marekani imetangaza vikwazo hivyo wakati ambapo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte yuko mjini Washington kwa mazungumzo na Trump.

Haya yanafanyika wakati ambapo urusi imeendeleza mashambulizi yake dhidi ya Ukraine kwa usiku wa pili mfululizo.

Shambulizi la usiku wa kuamkia leo limepelekea watu 4 kujeruhiwa na majengo katika wilaya kadhaa kuharibiwa mjini Kyiv.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW