1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yajiondoa katika Shirika la Afya Duniani

Dotto Bulendu
22 Januari 2026

Marekani inatarajiwa kujiondoa rasmi kwenye Shirika la Afya Duniani - WHO. Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus na wataalamu wengi wa afya duniani wamekuwa wakiihimiza Marekani kufikiria upya msimamo wake.

Rais Trump akisaini amri ya kuiondoa Marekani katika WHO mnamo Januari 20, 2025
Marekani imetahadharishwa kwamba kujiondoa kwenye WHO kutaawaathiri raia wake pamoja na mifumo ya afya ulimwenguni kotePicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Marekani imetahadharishwa kwamba hatua yake hiyo itaawaathiri wananchi wake pamoja na mifumo ya afya ulimwenguni kote pia imefahamishwa kuwa hatua hiyo inakiuka sheria ya Marekani inayoitaka serikali kulipa ada inayodaiwa na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa ya dola milioni 260.

Lawrence Gostin, mkurugenzi mwanzilishi wa Taasisi ya O'Neill ya Sheria ya Afya ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Georgetown huko mjini Washington, ambaye anafuatilia kwa karibu maswala yanayohusu shirika la WHO amesema hatua ya Marekani ni ukiukaji wa wazi wa sheria za nchi ingawa kuna uwezekano mkubwa kwa Trump kukiuka sheria na kuepuka kuwajibishwa.

Rais Donald Trump alitoa taarifa kwamba Marekani ingejiondoakutoka kwenye shirika hilo la afya duniani siku ya kwanza ya urais wake mnamo mwaka 2025, alipotia saini amri ya utendaji. Chini ya sheria ya Marekani, nchi hiyo inapaswa kutoa notisi ya mwaka mmoja na kulipa ada zote zilizobaki kabla ya kuondoka.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani amesema kushindwa kwa WHO kudhibiti, kusimamia na kushiriki taarifa kumeigharimu Marekani dola trilioni kadhaa na ndio sababu Rais Trump ametumia mamlaka yake kusitisha nchi yake kulipa fedha, kutoa msaada, au rasilimali zozote za serikali ya Marekani kwa WHO katika siku zijazo.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema Marekani kujiondoa ni hasara kwa kila mtuPicha: State House of Tanzania

Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ana matumaini makubwa Marekani itatafakari upya maamuzi yake haya na kuongeza kuwa uamuzi huo ni hasara kwa kila mtu

Miongoni mwa Shughuli ambazo Marekani ilikuwa inashiriki moja kwa moja na sasa haitashiriki tena ni pamoja na mifumo ya tahadhari ya mapema ya mlipuko wa magonjwa hatari,kuratibu utungaji wa chanzo za mafua baada yta kuchambua vinmelea vinavyozunguka duniani kote

Akizungumza na shirika la habari la Reuters huko Davos, mwenyekiti wa taasisi ya Gates Foundation, Bill Gates ambaye pia ni  mfadhili mkuu wa mipango ya afya ya kimataifa na baadhi ya kazi za WHO amesema hakutarajia Marekani kuchukua maamuzi hayo kwa  muda mfupi kiasi hiki.

Uamuzi huu wa Marekani sasa utailazimu WHO kufanya shughuli zake zikiwemo za utafiti na matibabu bila wataalamu kutoka Marekani ambao walikuwa mhimili ndani ya shirika hilo. Nchi wanachama zinatarajia kukutana mapema mwenzi ujao kujadili namna ya kuendesha shughuli za WHO bila uwepo wa Marekani.

Chanzo: Mashirika

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW