1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Marekani yalaani mauaji ya vikongwe 200 nchini Haiti

11 Desemba 2024

Marekani imelaani vikali mauaji ya takriban watu 200 yaliyofanywa na wanachama wa genge moja la uhalifu nchini Haiti.

Takriban watu 180 wengi wakiwa vikongwe wauawa Haiti.
Takriban watu 180 wengi wakiwa vikongwe wauawa Haiti.Picha: Guerinault Louis/Anadolu/picture alliance

Marekani  imelaani vikali mauaji ya takriban watu 200 yaliyofanywa na wanachama wa genge moja la uhalifu nchini Haiti.

Msemaji wa ikulu ya Marekani, Karine Jean-Pierre amesema ripoti ya kutokea mauaji hayo imeishtusha Marekani.

Siku ya Jumatatu ofisi ya waziri mkuu wa Haiti ilisema kwamba takriban watu 180 wengi vikongwe waliuwawa mwishoni mwa juma  katika eneo la Cite Soleil baada ya kushambuliwa.

Shirika moja lisilokuwa la kiserikali lilisema kwamba mashambulio hayo yaliamrishwa na kiongozi wa genge moja la wahalifu ambaye anashuku mwanawe amepata maradhi baada ya kufanyiwa mambo ya kishirikina.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW