1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yalaumiwa kwa mauwaji ya raia Somalia

16 Juni 2020

Ripoti mpya ya Shirika la Utetezi wa Haki za Binaadamu la Human Rights Watch inasema mashambulizi mawili ya anga yaliyofanywa na Marekani mapema mwaka huu yamewauwa raia saba nchini Somalia.

Somalia | Straßenbombe in der Nähe von Mogadischu  tötet 8 Zivilisten
Picha: Reuters/F. Omar

Shirika hilo la Human Rights Watch limesema jeshi la Marekani halikufanya uchunguzi wa kina kwa shambulizi lake la Februari 2, ambalo limemuuwa mwanamke mmoja akiwa nyumbani kwake. Na baadaye la Machi 10 ambalo limeangamizia maisha ya wanaume watano na mtoto mmoja.

Uchunguzi wa shirika hilo, haukubaini ushahidi wowote katika mashambulizi yote mawili, wa lengo la kijeshi katika kukabiliana na kundi la wenye itikadi kali za dini ya Kiislamu, lenye kujihami na silaha la Al-Shabab. Na wala si kamandi ya kijeshi ya pamoja kati ya Marekani na Afrika (AFRICOM) wala serikali ya Somalia wamewasiliana na familia kuchunga kwa lengo kuthibitisha kitendo hicho cha mauwaji ya raia au kutathmini madai hayo kwa lengo la kujirekebisha.

Ushihidi wa waathirika katika eneo la shambulizi

Muhanga wa shambulizi la bomu MogadishuPicha: AFP/A. H. Farah

Kati ya Februari na Mei, Human Rights Watch ilifanya mahojiano kwa njia ya simu na watu 14, wakiwemo ndugu na jamaa wa waliouwawa katika kipindi Februari na Machi. Wanne miongoni mwa hao walifika katika eneo la tukio, muda mfupi baada ya maafa na kutoa taarifa za kina.

Katika ripoti ya wa kuhusu kuhusu athari ya opereshini ya kivita nchini Somali kwa raia ya Aprili 27, mwaka huu AFRICOM ilisema ilichungumza matukio 20 ya anga ambayo yalidaiwa kusababisha maafa kwa wananchi kati ya Februri na Machi na kwamba katika kipindi hiki bado wanachunguza mengine saba. Miongoni mwa hayo ni pamoja ambayo shirika hilo la haki za binaadamu linasema limeyachunguza.

Katika hitimisho lake Human Rights Watch imetaka majeshi nchini Somalia kuacha mara moja kuwauwa raia wasio na hatia. Na kuyahimiza kuwatambua kwa ukamilifu wale wanaowalenga kabla ya kufanya mashambilizi.

Chanzo: HRW