1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Marekani yaliwekea vikwazo jeshi la Rwanda kutokana na mzozo

3 Machi 2026

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya jeshi la Rwanda na maafisa wanne waandamizi kwa tuhuma za kuliaunga mkono kundi waasi wa M23 Mashariki mwa Kongo.

Viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kusaini makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Rais wa Marekai Donald Trump 04.12.1015
Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa DRC, Felix TshisekediPicha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya fedha ya Marekani imefafanua kuwa watuhumiwa waliwasaidia waasi hao kupata udhibiti wa ardhi ikiwemo migodi muhimu mashariki mwa Kongo.

Matumaini ya kupata amani mashariki mwa Kongo yanazidi kufifia

Vikwazo hivyo vimetangazwa licha ya makubaliano ya amani yaliyosainiwa kati ya Rwanda na Kongo yaliyosimamiwa na Marekani.  Lakini hata baada ya makubaliano hayo, waasi wa M23 waliuteka mji wa Uvirana bado wanaendelea na operesheni zao katika eneo la mpaka na Burundi.

Serikali ya Rwanda imeikosoa hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo ikisema taifa hilo kubwa limeegemea upande mmoja, huku ikiilaumu Kongo kwa kushindwa kutekeleza makubaliano yanayolenga kuutatua mzozo huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW