1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Rais Joe Biden ampongeza Modi kwa kushinda uchaguzi

6 Juni 2024

Rais Joe Biden wa Marekani amempongeza Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa ushindi wa muungano wake wa kisiasa, akisema anatumaini wataendelea kushirikiana na kiongozi huyo wa Kihindu kwenye Asia iliyo huru.

India | Narendra Modi akutana na Joe Biden
Rais Joe Biden wa Marekani alipokutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kabla ya kuanza mazungumzo nchini India, Septemba 8, 2023Picha: Naveen Jora/Press Information/Planet Pix via ZUMA Press/picture alliance

Rais Biden ameandika kwenye mtandao wa X kwamba urafiki baina ya mataifa yao unazidi kuimarika katika wakati ambapo wanafungua fursa muhimu zaidi za kushirikiana huko siku za usoni.

Ikulu ya White House baadae ilitangaza kwamba mshauri wa masuala ya usalama Jake Sullivan atakwenda New Delhi kwa mazungumzo na serikai juu ya vipaumbele vya ushirikiano.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje nchini humo Matthew Miller alisema Marekani inatarajia kuimarisha zaidi ushirikiano na serikali ya India ili kukuza ustawi na  kushughulikia mzozo wa hali ya hewa.