Marekani yamshinikiza Aristide:
29 Februari 2004Matangazo
WASHINGTON/PORT-AU-PRINCE: Kufuatana na kuongezeka hali ya umwagaji damu nchini Haiti Marekani imeongeza mbinyo wake dhidi ya Rais Jean Bertrand Aristide. Mjini Washington tangazo la Afisi ya Rais linamlaumu kwa sehemu kubwa Rais Aristide kusababisha mgogoro wa sasa. Washington haina uhakika iwapo Rais huyo anaweza kuudhibiti mgogoro huo na kuendeleza utawala wake nchini Haiti, lilisema tangazo hilo. Rais Aristide amepinga tena madaia ya kujiuzulu yaliyotolewa na waasi ambao sasa wanadhibiti asili miya 70 ardhi ya Haiti. Hali ya fujo, machafuko na mauwaji imezidi kuongezeka katika mji mkuu Port-Au-Prince. Tangu Ijumaa wamekwisha uawa watu kumi mjini humo.
