1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Marekani yamtambua Urrutia kama rais mteule wa Venezuela

20 Novemba 2024

Marekani imesema inamtambua mgombea wa upinzani Edmundo Gonzalez Urrutia kama rais mteule wa Venezuela.

Mgombea wa upinzani nchini Venezuela Edmundo Gonzalez Urrutia
Mgombea wa upinzani nchini Venezuela Edmundo Gonzalez Urrutia Picha: Jeampier Arguinzones/dpa/picture alliance

Hii ni mara ya kwanza kumwita hivyo, ikiwa ni karibu miezi minne tangu ufanyike uchaguzi wenye utata.

Kauli hiyo ya Marekani imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje Anthony Blinken na imezusha hasira kali kutoka kwa serikali mjini Caracas, ambayo imeitaja kuwa "ujinga na upuuzi."

Soma pia: Bunge la Ulaya lamtambua Gonzalez rais halali Venezuela

Gonzalez Urrutia ameshukuru kwa kutambuliwa na Marekani akisema kuwa hiyo ni ishara inayoheshimu mabadiliko na maamuzi ya raia. Rais aliye madarakani Nicolas Maduro alidai kushinda uchaguzi huo wa Julai 28, ambao hata hivyo uligubikwa na shutuma nyingi za udanganyifu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW