Ombi la Ukraine la kutumia silaha za masafa marefu lakwama
7 Septemba 2024Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin ameondoa wazo la uwezekano wa kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za masafa marefu za Marekani kuyalenga maeneo ya ndani ya Urusi, akisema hilo haliwezi kubadili mwelekeo wa vita.
Austin ametoa kauli hiyo wakati wa kuhitimisha mkutano wa wadau wa kimataifa wanaoiunga mkono Ukraine uliofanyika katika kituo cha anga cha Marekani huko Ramstein nchini Ujerumani.
soma: Rais Zelensky kwa mara nyingine aomba silaha zaidi kupambana na Urusi
Mkuu huyo wa Pentagon, alisema Washington na washirika wake wataendelea kutoa msaada mkubwa kwa Ukraine katika kupambana na uvamizi wa Urusi, na kutangaza msaada mwingine wa dola milioni 250.
Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky aliyehudhuria mkutano huo, hapo awali aliwasilisha ombi la kupatiwa na kuruhusiwa kutumia silaha za masafa marefu kuyalenga maeneo ya ndani ya Urusi. Kiongozi huyo amewasili Italia jana jioni na atafanya mazungumzo na waziri mkuu Giorgia Meloni.