1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaongeza muda wa AGOA kwa mwaka mmoja

4 Februari 2026

Rais Donald Trump wa Marekani amesaini sheria ya kuongeza muda wa programu ya biashara yenye masharti nafuu kati ya nchi yake na Afrika hadi tarehe 31 Disemba mwaka huu.

Donald Trump
Rais Donald Trump wa Marekani ameongeza muda wa mwaka mmoja kwa mpango wa biashara na Afrika, maarufu kama AGOA.Picha: Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

Mwakilishi wa Biashara wa Marekani, Jamieson Greer, amesema ofisi yake sasa itashirikiana na Baraza la Congress mwaka huu ili kuifanya programu hiyo kutowa fursa zaidi za soko kwa ajili ya bidhaa, wakulima na wawindaji wa Marekani, ili kuendana na sera ya Marekani Kwanza ya Rais Trump.

Programu hiyo iitwayo kwa kifupi AGOA ilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 ili kutowa fursa ya soko lisilo ushuru kwa bidhaa za mataifa ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Ilifikia mwisho wake mnamo Septemba mwaka jana na kuhatarisha usalama wa nafasi za ajira kwa mamia kwa maelfu ya Waafrika.

Licha ya mwezi uliopita, Baraza la Wawakilishi kupiga kura ya kuiongezea muda wa miaka mitatu, Baraza la Seneti iliupunguza hadi kuwa mwaka mmoja tu, unaoishia mwishoni mwa mwaka huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW