1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaonya juu ya ukiukwaji wa makubaliano Sudan

Hawa Bihoga
26 Mei 2023

Marekani imesema mpango wa kuratibu usitishwaji wa mapigano nchini Sudan umegundua uwezekano wa ukiukwaji wa makubaliano hayo ikiwa ni pamoja na kushuhudiwa kwa mapigano katika miji ya Khartoum na Darful.

USA Washington Außenminister Antony Blinken
Picha: Mandel Ngan/AFP

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller aliwaambia waandishi wa habari kwamba Marekani imeendelea na mazungumzo ya faragha na pande zote mbili za mzozo huo, na kuongeza kuwa Washington haitasita kutumia zana zote zilizopo ili kuwawajibisha wahusika.

Mapigano ya hapa na pale kati ya jeshi laSudan na kikosi cha wanamgambo yameshuhudiwa hadi Alhamisi, na kusababisha hali ya utulivu katika mji mkuu Khartoum kutetereka na kuongeza hatari ya makubaliano ya usuluhishi ya wiki moja kuvunjika huku wasiwasi ukiongezeka juu ya mzozo wa kiutu.

Soma pia:Pande hasimu Sudan zalaumiana kukiuka usitishaji wa mapigano

Miller amewaambia waandishi wa habari mjini Washingoton kwamba, taarifa za uratibu wa kusitisha mapigano zimethibitisha kwamba mashambulizi ya anga na mapigano endelevu yameshuhudiwa katika eneo la viwanda la Khartoum.

Amesema mapigano mengine yamearifiwa huko Zalingei, katikati mwa Darfur na kusisitiza hawatasita kuchukua hatua zaidi hata kuweka vikwazo ikiwa tu makubaliano hayatadumishwa.

"Hakuna suluhu ya kijeshi katika mzozo huu." Afisa huyo wa marekani aliwaambia waandishi wa habari.

Alisisitiza kwamba hadi sasa wanaendelea, kushirikiana na pande zote kwa faragha, ili kuwalazimisha kuheshimu hali hiyo.

"Hatutasita kutumia zana zote zinazopatikana kwetu kuwawajibisha, ikibidi." Alisisitiza kauli hiyo ambayo iliwahi pia kutolewa na waziri wa Mambo ya nje Athony Blinken.

Kuafikiwa kwa usitiswahi wa vita kwa juma moja

Usitishaji huo wa mapigano unaoratibiwa na Saudi Arabia na Marekani, ulifikiwa baada ya wiki kadhaa za vita huko Khartoum na miripuko ya mapigano katika maeneo mengine ya Sudan, likiwemo eneo la magharibi mwa Darfur ambalo ni tete kiusalama kwa muda mrefu.

Mapigano hayo ambayo yaliyojikita zaidi katika mzozo wa madaraka kati ya jeshi la Sudanna Kikosi maalum cha wanamgambo yamezidisha mzozo wa kibinadamu, na kuwalazimu zaidi ya watu milioni 1.3 kuyakimbia makaazi yao ikiwa ni pamoja na zaidi ya 840,000 ambao wametafuta hifadhi maeneo salama ndani ya nchi na wengine 250,000 walivuka mpaka hadi nchi jirani, hii ikiwa ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Soma pia:Sudan: Makabiliano yaripotiwa baada ya kuanza usitishwaji mapigano kwa wiki moja

Hata hivyo mashirika ya kiraia nayo yanakadiria kuwa huenda idadi ya waliopoteza maisha ikaongezeka huku yakisisitiza kwamba takriban  3,530 walijeruhiwa katika mapambano hayo ya kuwania madaraka katika taifa hilo masikini la kusini mwa Afrika.

 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW