1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yapanga mkutano na Japan na Korea Kusini

Hawa Bihoga
1 Aprili 2024

Marekani inapanga mkutano wa kilele kati ya Rais Joe Biden na viongozi wenzake wa Japan na Korea Kusini mnamo mwezi Julai kandoni mwa mkutano wa Jumuiya ya NATO utaofanyika mjini Washington.

Rais wa Marekani Joe Biden, Fumio Kishida wa Japan na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol
Rais wa Marekani Joe Biden, Fumio Kishida wa Japan na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk YeolPicha: Andrew Harnik/AP/dpa/picture alliance

Taarifa za kuwepo kwa mkutano huo zimeripotiwa hii leo na vyombo vya habari vya Japan.

Miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kujadiliwa na viongozi hao ni pamoja na kuimarisha uwezo wa kuzuia ushawishi wa China unaoongezeka, kitisho cha nyuklia cha Korea Kaskazini na mahusiano ya kijeshi kati ya mataifa hayo na Urusi.

Soma pia: NATO yajitenga na kauli ya Macron ya kuingiza jeshi Ukraine

Hata hivyo si Japan wala Korea Kusini ambayo imethibitisha juu ya mkutano huo na Marekani.

Agosti mwaka jana, Rais Joe Biden wa Marekani aliwaalika viongozi wa Japan na Korea Kusini kwa mazungumzo sawa na hayo ambapo watatu hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi na kufanya mikutano ya kila mwaka.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW