1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yapanua kambi ya jeshi Kenya kuimarisha usalama

30 Januari 2026

Marekani imezindua mradi wa upanuzi wa njia ya kurukia ndege wenye thamani ya dola milioni 70 katika kambi ya jeshi la anga ya Manda Bay iliyoko kaunti ya Lamu karibu na mpaka na Somalia.

Marekani New York 2025 | Christopher Landau
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Christopher LandauPicha: Yuki Iwamura/AP Photo/picture alliance

Wakati wa hafla ya kuweka msingi wa mradi huo hapo jana, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani  Christopher Landau, alisema lazima wawaonyeshe wale wanaopanga kushambulia kwamba wamedhamiria kujilinda.

''Kambi hii inaonyesha dhamira inayoonekana wazi,  ulinzi wa pamoja kati ya Marekani na Kenya. Inatoa ishara kali kwa wale wanaopanga kuwa maadui zetu.''

Kambi hiyo ya Manda Bay hutumiwa na vikosi vya Marekani na kwa muda mrefu imekuwa kitovu cha kimkakati katika vita dhidi ya kundila Al-Shabaab lenye mafungamano na Al-Qaeda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW