MigogoroKorea Kusini
Marekani yapeleka ndege zaidi za kivita Korea Kusini
30 Agosti 2023Matangazo
Kulingana na wizara ya ulinzi ya Korea Kusini, ndege hizo zimeruka kwa pamoja na ndege za FA-50 za Korea Kusini kama sehemu ya luteka hizo za kijeshi. Ndege hizo pia ziliungana na zengine 12 za kivita kutoka Japan.
Marekani imetuma ndege hizi zilizo na uwezo wa kurusha mabomu siku chache baada ya Korea kaskazini kujaribu kurusha setlaiti, zoezi lililotibuka. Marekani na Korea Kusiniwalianza mazoezi hayo ya kijeshi waliyoyapa jina Ngao ya Uhuru ya Ulchi wiki iliyopita.
Lengo la mazoezi hayo ni kuzidisha jawabu lao kwa kitisho cha Korea Kaskazini kinachoongezeka cha makombora ya nyuklia. Sehemu ya pili ya mazoezi hayo yataanza Jumatatu ijayo.