Marekani yapewa mwezi mmoja kuokoa mazungumzo ya amani
9 Oktoba 2010Matangazo
Mawaziri hao wa mambo ya nje waliokutana katika mji wa Sirte nchini Libya wamesema, uamuzi huo umepitishwa ili kuzuia kuvunjika kwa majadiliano ya ana kwa ana yaliyoanzishwa upya kati ya Waisraeli na Wapalestina, mwanzoni mwa mwezi wa Septemba.
Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas alisitisha majadiliano hayo baada ya Israel kukataa kurefusha muda wa kusitisha ujenzi wa makaazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi.Muda huo ulimalizika mwisho wa mwezi wa Septemba.