1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yapinga azimio la UN kulaani ghasia dhidi ya raia

Sylvia Mwehozi
19 Oktoba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limeshindwa kupitisha azimio la kulaani ghasia dhidi ya raia katika vita vya Israel na Hamas na kuhimiza msaada wa kibinadamu kwa Wapalestina

Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield Picha: Fatih Aktas/Anadolu/picture alliance

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limeshindwa kupitisha azimio la kulaani ghasia dhidi ya raia katika vita vya Israel na Hamas na kuhimiza msaada wa kibinadamu kwa Wapalestina, baada ya Marekani kupinga azimio hilo ikisema ni mapema mno kuandaa azimio mwafaka la Baraza la Usalama katika mgogoro huo.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield alisema baraza hilo linahitaji kuruhusu juhudi za sasa za kidiplomasia na kutafuta ukweli zaidi wa kile kinachoendelea.Baraza la Usalama kupiga kura juu ya mzozo wa Israel-Gaza

Aidha, Balozi huyo alikosoa hatua za kushindwa kusisitiza haki ya Israel kujilinda. Azimio hilo lililoandaliwa na Brazil lilikuwa na uungwaji mkono mkubwa na lingelaani ghasia zote dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na mashambulio mabaya ya wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW