1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yarejea UNESCO baada ya kujitoa kwa miaka 6

1 Julai 2023

Marekani imerejea kuwa mwanachama wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, miaka 6 tangu ilipojiondoa wakati wa utawala wa rais Donald Trump.

Logo | Unesco
Picha: Alain Jocard/AFP/dpa/picture alliance

Kikao maalum cha Baraza Kuu la UNESCO kimepiga kura kwa wingi kuijeresha Marekani ndani ya shirika hilo licha ya upinzani kutoka Urusi na China. Mataifa mengine yaliyopinga azimio hilo  ni Iran, Syria, na Korea Kaskazini.

Soma zaidi:Marekani yajiondoa uanachama UNESCO

Rais wa zamani wa Marekani alioondoa rasmi nchini hiyo ndani ya UNESCO mnamo mwaka 2018 akilituhumu shirika hilo kuwa na chuki dhidi ya Israel.

Marekani ambayo ni moja ya wanachama waanzilishi wa shirika hilo ilikuwa mchangiaji mkubwa wa bajeti ya UNESCO hadi mwaka 2011 pale shirika hilo lilipoikaribisha Palestina uamuzi uliozusha ukosoaji kutoka Washington.