1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaridhishwa na usambazaji misaada Sudan

Josephat Charo
1 Oktoba 2024

Marekani imesema imeridhishwa na usambazaji wa misaada katika nchi inayokubwa na vita ya Sudan. Malori ya misaada yameanza kupitia maeneo ambako kulikuwa hakupitiki kutokana na mapiganao.

Mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya Sudan, Tom Perriello, kushoto.
Mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya Sudan, Tom Perriello, kushoto.Picha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/picture alliance

Mjumbe maalumu wa Marekani nchini Sudan Tom Perriello amesema upelekaji wa misaada ya kibinadamu umeboreka kwa kiwango kikubwa nchini humo.

Perriello amewaambia waandishi habari mjini Nairobi, Kenya kwamba wana mamia kadhaa ya malori ya misaada yanayopita na kufika maeneo ambako awali kulikuwa kumefungwa kutokana na machafuko.

Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa zaidi ya watu milioni 25 wanakabiliwa na njaa kali huku baa la njaa likitangazwa katika kambi ya watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao katika eneo la magharibi la Darfur linalopakana na Chad.

Perriello amesema hali ni mbaya sana na wale walio katika nafasi nzuri kabisa ya kuizuia wanaonekana kuwa na ari ya kuichochoea izidi kuwa mbaya.

Vita vya Sudan vilizuka mnamo Aprili 2023 na vimewaua maalfu ya watu huku shirika la afya duniani WHO likitangaza vifo vya watu wapatao 20,000 lakini makadirio mengine yakiiweka idadi ya vifo kufikia 150,000.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW