1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yasaka chanzo cha kuvuja kwa nyaraka zake za siri

11 Aprili 2023

Maafisa wa Marekani wanapambana kubaini chanzo cha kuvuja kwa nyaraka za siri, kupitia mitandao ya kijamii, ambazo zina maudhui kuhusiana na mfumo wa kujilinda angani wa Ukraine, idara ya usalama ya Israel na China.

USA Washington D.C. | US-Verteidigungsminister Lloyd Austin spricht bei virtuellem Treffen der Ukraine Defense Contact Group
Picha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP/Getty Images

Msemaji msaidizi wa idara ya mahusiano katika wizara ya ulinzi ya Marekani, Chris Meagher, aliwaambia waandishi wa habari jana Jumatatu kwamba uvujaji huo unawakilisha kitisho kikubwa kabisa dhidi ya usalama wa taifa.

Amesema,  Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin  amewasiliana na washirika wao kuangazia kisa hicho tangu kilipotokea Alhamisi iliyopita.

Mitandao ya Twitter, Telegram, Discord na mingineyo imekuwa ikizipata nyaraka hizo katika siku chache zilizopita na nyingine mpya zinaendelea kuingia.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, amekitaja kisa hicho kama cha kuvutia, huku akipuuzia madai kwamba huenda Moscow inahusika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW