1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Marekani yasambaratisha makombora ya waasi wa Houthi

17 Januari 2024

Jeshi la Marekani limefanya mashambulizi mengine dhidi ya miundombinu ya waasi wa Houthi wa nchini Yemen, saa chache baada ya kombora kuipiga meli ya mizigo inayomilikiwa na Ugiriki iliyokuwa inakatisha Bahari ya Shamu.

Yemen | Sanaa | Silaha | Waasi wa Houthi
Moja ya silaha zinazotumiwa na waasi wa Houthi wa nchini Yemen Picha: Mohammed Mohammed/Xinhua News Agency via picture alliance

Ikulu ya Marekani imesema mashambulizi hayo ya jana jioni yamesambaratisha makombora ya masafa ya waasi wa Houthi ambayo inashuku yaliyokuwa tayari kutumika kuzilenga meli za mizigo.

Yalifanyika baada ya meli nyingine ya mizigo kushambuliwa na waasi wa Houthi ikiwa safarini kutokea Vietnam kwenda nchini Israel. Msemaji wa waasi wa Houthi amethibitisha kuwa waliilenga meli hiyo iitwayo Zografia ikiwa umbali wa maili 76 za baharini kutoka bandari ya Saleef ya nchini Yemen.

Kwa wiki kadhaa sasa kundi hilo la waasi limekuwa likizilenga meli kwenye ujia wa Bahari Nyekundu likisema ni kwa dhima ya kuishinikiza Israel isitishe mashambulizi yake huko Ukanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW