Marekani yasema Israel haijajiandaa kuishambulia Rafah
9 Februari 2024Matangazo
Msemaji wa wizara hiyo, Vedant Patel. amewaambia waandishi wa habari kwamba operesheni kama hii kwa wakati huu bila ya mipango katika eneo linalowahifadhi watu milioni moja itakuwa ni janga.
Soma zaidi: Blinken amaliza ziara ya Mashariki ya Kati baada ya Israel kukataa pendekezo la kusitisha vita
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema siku ya Jumatano kwamba vikosi vya Israel vilikuwa vinajiandaa kuushambulia mji wa Rafah, ulioko kwenye mpaka na Misri.
Watu wengi wanaoishi kwenye mji huo waliyakimbia makazi yao katika Ukanda wa Gaza wakati Israel ikiendeleza mashambulizi yake ya dhidi ya wanamgambo wa Hamas.