1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema Israel kuongeza kivuko kuingiza misaada Gaza

8 Novemba 2024

Israel imeiarifu Marekani kwamba itafungua kituo cha nyongeza cha kuingiza misaada kwenye Ukanda wa Gaza.

Hali ya kiutu Gaza
Mashirika kadhaa ya kimataifa yanasema hali ya kiutu Gaza ni mbaya.Picha: Mahmoud Issa/Middle East Images/picture alliance

Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani kupitia msemaji wake Matthew Miller. Afisa huyo amesema baada ya hivi karibuni Israel kukifungua kivuko cha mpakani cha Erez, serikali mjni Tel Aviv inapanga kuongeza njia nyingine ya kuingiza misaada Gaza kwenye eneo la Kissifum.

Miller amesema Washington imeendelea kuwashinikiza viongozi wa Istael na kwamba wameonesha kuchukua hatua kushughulikia wasiwasi ulioelezwa na Marekani juu ya kuzorota hali ya kutu kwenye Ukanda wa Gaza.

Taarifa hiyo imetolewa katika wakati muda wa mwisho uliowekwa na Washington wa kuboreshwa hali ya kiutu kwenye eneo hilo unakaribia  wiki inayokuja.

Mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa Marekani waliipa Israel hadi Novemba 13 kuboresha hali ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza au misaada kadhaa ya kijeshi kutoka Washington itazuiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW