Marekani yasema jeshi liko tayari kuchukua hatua
16 Aprili 2026
Jeshi la Marekani Mashariki ya Kati limesema liko tayari kuanza tena mapigano mara moja ikiwa Iran haitakubali makubaliano ya amani.
Kwa mujibu wa maafisa wa juu wa kijeshi wa Marekani hatua hiyo ni sehemu ya shinikizo kwa Tehran kusaini mkataba, huku vikosi vyake vikianzisha zuio dhidi ya meli zote zinazoingia au kutoka Iran.
Waziri wa Ulinzi, Pete Hegseth, amesema Iran ina nafasi ya kuchagua mustakabali wenye ustawi kwa wananchi wake, lakini akaonya kuwa ikikataa, itakumbana na mashambulizi yatakayolenga miundombinu, nishati na umeme.
Mkuu wa Majeshi ya Pamoja, Jenerali Dan Caine, amesema vikosi vya Marekani viko tayari kuanza operesheni kubwa za kijeshi wakati wowote. Ameongeza kuwa meli za kijeshi zitazuia au kukamata meliyoyote inayojaribu kuvunja zuio hilo, na zitatumia nguvu endapo hazitatii.
Hadi sasa, meli 13 zimerudi nyuma badala ya kuvunja zuio hilo, hakuna meli iliyokamatwa kufikia sasa.