SiasaEthiopia
Marekani: Uhalifu wa kivita ulifanywa katika vita vya Tigray
21 Machi 2023Matangazo
Akizungumza wakati akiwasilisha ripoti ya uchunguzi, Waziri wa Mambo ya Kigeni Antony Blinken amesema kuwa wale waliohusika lazima wawajibishwe.
Ripoti hiyo inaweka uzito kwa tuhuma za awali kuhusiana na uhalifu uliofanywa, na kutoa wito wa kufunguliwa mashitaka. Ripoti hiyo ya kila mwaka ya haki za binaadamu pia ilisema pande zote isipokuwa tu Jeshi la Ukombozi wa Watu wa Tigray - TPLF zilihusika na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.
Soma pia: Blinken aiomba Ethiopia kuimarisha amani baada ya vita
Blinken amesema uhalifu huo ni pamoja na mauaji, ubakaji, na aina nyingine za ukatili wa kijinsia pamoja na mateso. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, vita hivyo inaaminika vilisababisha mamilioni ya wakimbizi wa ndani.