1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani: Ushirikiano na Niger ni wa manufaa kwa pande zote

Hawa Bihoga
19 Machi 2024

Marekani imeuelezea uhusiano wake wa kijeshi na Niger kama wa manufaa kwa pande zote, wakati ikisubiri ufafanuzi kuhusu tangazo la kuvunja uhusiano huo.

Wanajeshi wa Marekani wakiwa na wenzao wa Niger wakiwa katika luteka za pamoja.
Wanajeshi wa Marekani wakiwa na wenzao wa Niger wakiwa katika luteka za pamoja.Picha: Alex Fox Echols Iii/Planetpix/Planet Pix via ZUMA Wire/picture alliance

Jeshi la Niger, ambalo lilitwaa madaraka Julai mwaka jana, lilitagaza Jumamosi jioni kwamba lilikuwa linasitisha makubaliano na Marekani mara moja, lakini wanadiplomasia wanasema kulikuwepo na ujumbe mchanganyiko usio rasmi. 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Vedant Patel, alisema walikuwa wanawasiliana na utawala wa mpito kupata ufafanuzi juu matamshi yao na kujadili hatua zinazofuata. 

Soma pia:Marekani yatathmini mustakabali wa operesheni zake Sahel.

Niger, ambayo ni mmoja ya mataifa ya maskini zaidi duniani, ilikuwa mshirika wa karibu wa mataifa ya magharibi katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa itikadi kali katika kanda ya Sahel, ambapo Marekani ilijenga kituo kikubwa cha droni kilichogharimu dola milioni 100.