1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Marekani yashambulia ngome 15 za Wahouthi, Yemen

5 Oktoba 2024

Jeshi la Marekani linasema vikosi vyake vimefanya mashambulizi katika maeneo 15 yanayodhibitiwa na Wahouthi huko Yemen.

Meli ya mafuta iliyoshambuliwa na Wahouthi katika bahari ya Shamu, Yemen
Meli ya mafuta iliyoshambuliwa na Wahouthi katika bahari ya Shamu, YemenPicha: Eunavfor Aspides/HO/AFP

Kulingana na televisheni ya wanamgambo wa Houthi Al Masirah, mashambulizi hayo yamelenga maeneo 4 tu.

Marekani na Uingereza zimekuwa zikifanya mashambulizi yenye lengo la kuusitisha uwezo wa Wahouthi kuzishambulia meli, ila mashambulizi ya waasi hao kwa meli zinazopitia Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden, yameendelea.

"Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) imefanya mashambulizi ikilenga ngome 15 za Wahouthi katika maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi nchini Yemen," ilisema kamandi hiyo katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii.

Wapiganaji wa Kihouthi Sanaa, YemenPicha: Yahya Arhab/EPA

Mashambulizi tangu Novemba

Televisheni ya Al Masirah iliyosema Marekani na Uingereza zote ziliishambulia Yemen Ijumaa, awali ilikuwa imeripoti mashambulizi 4 huko Sanaa na mengine 7 Hodeida. Waandishi wa shirika la habari la Ufaransa AFP, wamesikia milipuko mikubwa katika hiyo miji yote miwili.

Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran wamekuwa wakizishambulia meli katika njia hiyo tangu mwezi Novemba wakidai lengo lao ni meli zilizo na mafungamano na Israel na mashambulizi hayo yanalenga kuonyesha mshikamano na Wapalestina wakati wa vita vya Israel dhidi ya Hamas huko Gaza.

Israel pia imeishambulia Yemen kutokana na hayo mashambulizi ya Wahouthi.

Moto kutokana na shambulizi la Israel Hodeida, YemenPicha: Social Media/via REUTERS

Mashambulizi ya Israel Hodeida mwezi uliopita yalisababisha vifo vya angalau watu 5 baada ya waasi hao kusema kwamba waliulenga kwa kombora uwanja wa ndege wa Ben Guiron nchini Israel.

Vyanzo: AFPE/AP