1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Marekani yashtushwa na wizi wa chakula Ethiopia

Josephat Charo
29 Juni 2023

Marekani inasema imeshtushwa na hali nchini Ethiopia baada ya wizi kusababisha upelekaji wa misaada ya chakula kusitishwa na vifo.

UN berichtet über Welthunger
Picha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Shirika la misaada la Marekani USAID limeliambia shirika la habari la Associated Press haliridhirishwi na hali ya Ethiopia ambako maafisa wameripoti kutokea vifo kutokana na njaa katika wiki chache zilizopita baada ya Marekani na Umoja wa Mataifa kusitisha msaada wa chakula kutokana na wizi.

Maafisa wa Marekani wameshasema kibinafsi kwamba huu huenda ukawa wizi mkubwa kabisa wa chakula cha msaada kuwahi kutokea katika nchi yoyote duniani.

Marekani na Umoja wa Mataifa bado hawajasema ni nani aliyehusika na wizi huo uliogunduliwa kwa mara ya kwanza mwezi Machi katika eneo la kaskazini la Tigray, wakati tani za vyakula vya msaada kwa ajili ya watu wenye mahitaji zilipopatikana zikiuzwa kwenye magunia yaliyokuwa na alama ya bendera ya Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW