Marekani yaitaka Kongo kutatua 'mzozo wa uchaguzi' kwa amani
1 Januari 2024Matangazo
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema kuwa Washington inafuatilia mchakato huo kwa ''karibu'' bila ya kutoa mara moja pongezi zake kwa Tshisekedi.
Msemaji huyo ameendelea kusema kuwa "mizozo yoyote ya uchaguzi inapaswa kutatuliwa kwa amani na kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Kongo'' na akatoa wito kwa mamlaka husika ''kuhakikisha malalamiko yoyote yanashughulikiwa kwa haki na uwazi."
Matokeo ya awali yanaonesha kuwa Tshisekedi ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 73 ya kura, ambazo tayari viongozi wa upinzani wamezipuuza na kuzitaja kuwa ni "za uongo."
Mahakama ya kikatiba ya Kongo inatarajiwa kuthibitisha matokeo hayo ya awali mnamo Januari 10.