1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yataka ulinzi wa baharini eneo la Iran na Yemen

10 Julai 2019

Marekani imetoa wito kwa mataifa kuunda umoja wa kulilinda eneo la bahari la Iran na Yemen. Mpango huo utalifanya taifa hilo kuchukua jukumu muhimu la uongozi wa operesheni ya kijeshi na jukumu la kiintelijensia.

US-Drohne Global Hawk
Picha: picture-alliance/US Air Force/Zumapress

Jeshi la Marekani linakusudia kuunda muungano wa jeshi la wanamaji, ambao utahakikisha uhuru wa safari za majini, katika maeneo ya kimkakati ya rasi ya Uarabuni. Marekani inailaumu Iran kwa kujifungamanisha na makundi yanayofanya matukio ya mashambulizi ya meli za kibiashara. Na kutilia mkazo kwamba eneo la bahari la Iran na Yemen linapaswa kuwa salama.

Katika mpango huo, uliotangazwa jana, Marekani itaweka utaratibu wa uangalizi wa eneo la bahari sambamba na ufuatiliaji wake, wakati kila taifa mwanachama katika muungano huo, litatoa ulinzi wa meli zake za kibiashara ambazo zinasafiri kwa kupeperusha bendera  ya taifa husika.

Mataifa washirika kupaswa kusindikiza meli zao

Meli ya mafuta katika bahari ya Ghuba ya OmanPicha: picture-alliance/AP Photo/ISNA

Doria itafanyika, hasa katika maeneo tete ya bahari kama maeneo ya ujia wa bahari wa Hormuz, unaoligawa eneo laGhuba ya Iran na Oman. Vilevele jitihada za ulinzi zitalizingatia eneo lingine la Bab el Mandeb, ambalo linaigawa Yemen kutoka katika eneo la Pembe ya Afrika.

Kwa mujibu wa DW Jenerali wa jeshi la majini wa Marekani Joseph Danford, ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya pamoja ya wakuu wa vikosi amesema kwa hivi sasa wanayahusisha mataifa kwa idadi yao, ili kuweza kufanikisha uundwaji wa jeshi la pamoja kwa shabaha ya kuyaweka maeneo hayo lengwa katika hali ya usalama zaidi.

Mpango kubainikia wiki chache zijazo

Aidha Jenerali Danford aliongeza kwa kusema anafikiri katika kipindi cha wiki kadhaa zijazo, wanaweza kubaini taifa gani miongoni mwa mataifa lengwa lina utashi wa kisiasa, kuunga mkono jitihada hiyo, alafu baada ya hapo watafanya kazi na majeshi ili kuweza kutambua uwezo uliopo katika kutekeleza lengo.

Karibu robo tatu ya kiwango cha mafuta ya ulimwengu usafirishwa kwa njia  hiyo ya bahari, ambayo katika majuma ya hivi karibuni imezuisha mivutano. Marekani inaishutumu Iran kwa mashambulizi ya meli za shehena za mafuta, wakati serikali ya Iran pia ilidungua ndege inayoruka bila ya rubani yya ukaguzi wa usalama katika maeneo hayo.

Mwezi uliopita Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo alisema ana matumani zaidi ya mataifa 20 yatafanya kazi kwa pamoja katika kuimarisha usalama wa eneo la bahari katika eneo hilo, ikijumuisha Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudia Arabia.

Chanzo: DW