Marekani yataka uwazi katika udhibiti wa silaha za nyuklia
4 Mei 2010Matangazo
Msemaji wa wizara hiyo, Dave Lapan amesema Marekni kwa kufichua idadi ya silaha zake, iliyowekwa siri hadi sasa, inataka kuhimiza uwazi katika jitahada za kuzuia utapakaaji wa silaha za nyuklia duniani.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton alipozungumza katika mkutano wa kuzuia utapakaaji wa silaha za nyuklia mjini New York alisema, Iran inayoendelea na mradi wake wa nyuklia inadharau kanuni za kimataifa na ametoa wito wa kuichukulia hatua kali.
Nae Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad alipotoa hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, aliituhumu Marekani kuwa inatumia silaha zake za nyuklia kuishinikiza Iran. Wajumbe wa Marekani na nchi kadhaa za Ulaya walitoka nje ya ukumbi huo.