1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatangaza mpango wa ulinzi katika bahari ya Shamu

19 Desemba 2023

Marekani na mataifa mengine kadhaa yanaunda jeshi ili kuzilinda meli zinazopita kwenye bahari ya Shamu ambako zimekuwa zinashambuliwa kwa droni na makombora kutokea maeneo ya nchini Yemen yanayodhibitiwa na Wahouthi.

Lloyd Austin trifft israelischen Premierminister Netanyahu in Tel Aviv
Picha: Chad Mcneeley/Dod/picture alliance

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, amesema hayo nchini Bahrain.

Ukubwa wa mashambulio hayo ambayo baadhi yameharibu vyombo vya baharini, yamesababisha kampuni kadhaa za usafirishaji kuchukua hatua za kuepusha meli zao kupitia kwenye mlango wa bahari wa Bab el-Mandeb hadi hali ya usalama itakaposhughulikiwa.

Chini ya mkakati huo mpya meli za kijeshi zitaongeza uwepo wake kwenye eneo la bahari hiyo  ya Shamu na kujiweka katika namna ya kuweza kuzilinda meli za biashara.     

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW