1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Marekani yatangaza msaada mpya wa dola milioni 160 kwa Haiti

26 Septemba 2024

Marekani imetangaza msaada mpya wa dola milioni 160 kuisaidia Haiti, ambako kumetumwa pia kikosi cha kimataifa cha kulinda amani ili kujaribu kuleta utulivu katika nchi hiyo inayokumbwa na ghasia za magenge ya wahalifu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Roberto Schmidt/Pool/AP Photo/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye alifanya ziara katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince mapema mwezi huu ametoa tangazo hilo pembezoni mwa mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Mkutano huo ulihudhuriwa na  Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille , rais wa baraza la mpito Edgard Leblanc Fils, pamoja na mawaziri kutoka Kenya, Canada, Ufaransa, na wanachama wa Jumuiya ya nchi za Caribbean (Caricom).

Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari, msaada huo utatumiwa kwenye sekta ya maendeleo, uchumi, afya na usalama kwa watu wa Haiti, na hivyo kupelekea msaada wa Marekani kwa nchi hiyo ya Caribbean kufikia hadi dola bilioni 1.3 tangu mwaka 2021.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW