Marekani yatangaza msaada mpya wa kijeshi kwa Ukraine
11 Oktoba 2023Tukianza na uungwaji mkono wa Ukraine ni kwamba waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, ametangaza msaada mpya wa kijeshi wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 200 na kufanya msaada jumla uliotolewa na Marekani kufikia dola bilioni 43.9. Msaada huo unajumuisha silaha za mifumo ya ulinzi wa anga, silaha za angani na makombora pamoja na vifaa vya kuzidungua ndege za droni za Urusi. Austin ameapa kwamba "Marekani itaendelea kusimama na Ukraine kadri itakavyohitajika".
Uungwaji mkono wa NATO: NATO: Tunaendelea kuiunga mkono Ukraine
"Ukraine inapiga hatua kusNATO: Tunaendelea kuiunga mkono Ukraineonga mbele. Na inaendelea kukomboa maeneo muhimu kutoka kwa wavamizi wa Urusi. Haya ni mapambano makali na hatari. Na tunawapongeza wananchi wa Ukraine wenye ujasiri wa kuhatarisha maisha yao ili kulirudisha nyuma jeshi la kichokozi la Putin. Ni lazima tuendelee kuisadiia Ukraine na kile inachohitaji ili kukabiliana na changamoto za sasa, na hata kuendelea kukuza uwezo wake wa kupambana ili kuepusha hatari katika siku zijazo," alisema Austin.
Tangazo la Austin linatolewa baada ya kuwepo na mashaka kwamba vita vya Israel dhidi ya kundi la Hamas, vinaweza kuchepusha mwelekeo wa Washington katika kuisadia Kyiv. Waziri huyo wa ulinzi wa Marekani ametoa tangazo hilo wakati alipofungua mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa NATO mjini Brussels, ambako Rais Volodymyr Zelensky amehudhuria.
Ubelgiji nayo imetangaza kuwa itapeleka ndege za kivita chapa F-16 kwa Ukraine kuanzia mwaka 2025 ikiwemo pia kuzikarabati ndege na mafunzo kwa maafisa wa Ukraine. Hayo yameelezwa na waziri mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo baada ya kukutana na Zelensky.
Ukiacha suala la Ukraine, mawaziri hao wa ulinzi pia wanajadili sakata la uharibifu wa bomba la gesi na mtandao wa mawasiliano kati ya nchi wanachama za Finland na Estonia. Mwishoni mwa juma wataalamu wa matetemeko walitoa taarifa ya kuwepo na dalili za uwezakano wa mlipuko ulioharibu bomba la gesi la chini ya bahari ya Baltiki linalounganisha Finland na Estonia. Taarifa hizo zilitihibitishwa jana na Finland iliyadai kwamba uharibifu huo umesababishwa na "shughuli za nje" na kuongeza wasiwasi juu ya usalama wa nishati wa kikanda na kupanda bei ya gesi.
Uanachama wa Finland NATO: Finland kujiunga rasmi na NATO siku ya Jumanne
Lakini hii leo Rais wa Estonia Alar Karis amesema bado hawajabaini nani amesababisha uharibifu huo. Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ameongezea kwamba ikiwa "itathibitishwa uharibifu huo ulikuwa ni shambulio la kukusudia dhidi ya miundombinu muhimu ya NATO basi litashughulikiwa vikali na jumuiya hiyo".