1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatangaza msaada wa kijeshi kwa Taiwan

Sylvia Mwehozi
29 Julai 2023

Marekani imetangaza msaada wa kijeshi wa Dola milioni 345 kwa Taiwan, katika hatua inayoweza kuikasirisha zaidi China, katika wakati ambao uhusiano wa mataifa hayo mawili umezidi kudorora.

Mazoezi ya ndege ya kijeshi ya Taiwan
Helkopita chapa AH-64 ikifanya zoezi kaskazini mwa TaiwanPicha: Chiang Ying-ying/AP Photo/picture alliance

Marekani imetangaza msaada wa kijeshi wa Dola milioni 345 kwa Taiwan, katika hatua inayoweza kuikasirisha zaidi China, katika wakati ambao uhusiano wa mataifa hayo mawili umezidi kudorora.

China, inayozidi kujiimarisha kidiplomasia na kijeshi, inadai kwamba kisiwa cha Taiwan kinachojitawala kidemokrasia, ni sehemu yake na imeapa kukitwaa kwa nguvu ikibidi.

Mvutano umeongezeka huku China ikifanya mazoezi ya mara kwa mara ya ndege za kivita na meli kuzunguka kisiwa hicho, huku Marekani ikionekana kujaribu kuipatia nguvu za kijeshi Taiwan ili kuzuia uvamizi unaoweza kujitokeza.

Afisa mmoja wa Marekani aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina alidokeza siku ya Ijumaa kwamba, msaada huo utajumuisha vifaa vya kijasusi, uchunguzi na upelelezi sambamba na silaha ndogondogo. Bunge la Marekani liliidhinisha Rais Joe Biden kutoa msaada kijeshi kwa Taiwankama ilivyokuwa kwa Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW