1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya rais wa Zimbabwe

5 Machi 2024

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na maafisa wengine waandamizi wa nchi hiyo ikiwatuhumu kwa rushwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

 Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe
Rais Emmerson Mnangagwa wa ZimbabwePicha: Tsvangirayi Mukwazh/AP Photo/picture alliance

Tangazo hilo limetolewa jana na wizara ya fedha ya Marekani ambayo imesema vikwazo hivyo vinaulenga mtandao wa kihalifu unaojumuisha maafisa wakuu wa serikali chini ya rais Mnangagwa ambao umekuwa ukiwahujumu watu wa Zimbabwe.

Wale waliolengwa na vikwazo hivyo watazuiwa kufanya safari zisizo rasmi nchini Marekani na mali zao zitazuiliwa.

Kupitia tangazo hilo Marekani pia imesema inaondoa vikwazo jumla vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo la kusini mwa Afrika ambavyo vimedumu kwa karibu miongo miwili.

Vikwazo hivyo viliwekwa mnamo mwaka 2003 vikulenga utawala wa zamani wa Rais Robert Mugabe kufuatia sera yake ya ardhi iliyotaifisha mashamba makubwa yaliyokuwa yakimilikiwa na walowezi wa kizungu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW