1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Marekani: Ruksa Israel kuuza mfumo wa ulinzi kwa Ujerumani.

17 Agosti 2023

Wizara ya ulinzi ya Israel imesema Marekani imekubali nchi hiyo iuze kwa Ujerumani mfumo wa ulinzi aina ya Arrow 3, huu utakuwa mradi mkubwa kabisa wa ulinzi kuwahi kufikiwa.

Israel Arrow Raketensystem/Hatzor Luftstützpunkt
Picha: ZUMA/IMAGO

Wizara ya ulinzi ya Israel imeeleza kwamba makubaliano hayo yenye thamani ya Euro bilioni 3.5 utakuwa mradi mkubwa kabisa wa ulinzi kuwahi kufikiwa.

Ridhaa ya Marekani inazingatiwa kuwa hatua ya kuondolewa kikwazo cha mwishokatika njia ya kufikia mapatano juu ya masuala ya ulinzi baina ya Israel na Ujerumani. Mkataba huo utatiwa saini na wizara za ulinzi za nchi hizo mbili mwishoni mwa mwaka huu.

Soma piaIsrael yawashikilia wafungwa zaidi ya 1,200 bila mashtaka

Kamati za bajeti na ulinzi za bunge la Ujerumani zilipiga kura mwezi uliopita kuridhia mkataba huo. Mfumo wa ulinzi aina ya Arrow 3 uliundwa kwa pamoja baina yaIsrael na Marekanina unatarajiwa kuanza kutumika kwa ajili ya ulinzi wa Ulaya katika miaka miwili ijayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW