1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Marekani yatoa nyongeza ya mamilioni ya dola kuisaidia Sudan

Sylvia Mwehozi
19 Julai 2024

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield, ametangaza msaada wa ziada wa karibu dola milioni 203 kwa Sudan.

Sudan| Shida ya maji| Vita
Vita nchini Sudan vimesababisha ukosefu mkubwa wa chakula na maji. Picha: AFP

Licha ya msaada huo alioutangaza jana, Greenfield ameonya kuwa hilo siyo suluhisho la mzozo wa nchi hiyo.

Mwakilishi huyo wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amezitolea wito nchi wanachama, kutimiza ahadi zao kwa Sudan,inayokabiliwa na vita ili kushughulikia kile alichokiita mgogoro mbaya zaidi wa kiutu duniani.

Mwezi Aprili mwaka huu, viongozi wa dunia waliahidi kuichangia nchi hiyo zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 2.1,  katika mkutano wa wahisani uliofanyika mjini Paris.

Sudan, iliingia katika machafuko mwezi Aprili mwaka 2023 baada ya kuibuka mivutano kati ya kiongozi wa jeshi rasmi la nchi hiyo Abdel Fattah al Burhan na kikosi  cha wanamgambo wa RSF kinachoongozwa na Hamdan Dagalo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW