1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Marekani yatoa wito wa kuhuisha kikosi cha usalama Haiti

6 Septemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ametoa wito wa kuongezwa muda wa kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti kulisaidia taifa hilo kupambana na magenge yenye silaha kwenye mji mkuu wa Port au Prince.

Israel | US Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Kevin Mohatt/REUTERS

Muda wa miezi 12 wa kikosi hicho unamalizika mwanzoni mwa mwezi Oktoba, lakini kimekuwa na mafanikio madogo kutokana na kuwa na wanajeshi wachache na ufadhili duni.

Soma pia: Polisi wa Kenya nchini Haiti wakumbana na vikwazo

Antony Blinken amesema nchi yake, ambayo ndiyo mfadhili mkubwa wa kikosi hicho, ilipanga kuitisha mkutano wa mawaziri katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi huu, ili kuhimiza michango zaidi ya kifedha na kuongeza muda wa kikosi hicho nchini Haiti.

Kulingana na Blinken, wanachokihitaji ni kitu cha kuaminika na endelevu na watafanya kila njia kutimiza hilo.