1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yafuta makubaliano na washitakiwa wa tukio la 11.09

3 Agosti 2024

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema amevunja makubaliano na washitakiwa watatu waliohusishwa na mashambulizi ya Septemba 11, 2001, siku mbili baada ya kutangazwa kwake.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd AustinPicha: Alex Wong/Getty Images

Makubaliano hayo kati ya Marekani na Khalid Sheikh Mohammed na washitakiwa wengine wawili, yaliwataka kukiri mashtaka ili kufutiwa adhabu ya kifo na badala yake wahukumiwe kifungo cha maisha jela.

Soma pia:Washukiwa wa 9/11 wafikia mpango kupunguziwa adhabu

Washitakiwa hao wanazuiwa kwenye gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba, wanakabiliwa na makosa ya kula njama, ugaidi na mauaji ya watu 2,976 kufuatia mashambulizi kwenye kituo cha Kimataifa cha Biashara mjini Washington, Pentagon kwenyewe na uwanja wa Shanksville, Pennysylvania.