Marekani yaiondolea vikwazo vya usafiri Chad
11 Aprili 2018Kulingana na Ikulu ya White House, uchunguzi huo uligundua kuwa taifa hilo lililoko Afrika ya Kati lilikuwa limeimarisha viwango vya usalama na utoaji wa mawasiliano kuhusu raia wake kwa Marekani.
Chad ilikuwa miongoni mwa nchi nane zilizolengwa na vikwazo vya usafiri kwa raia wake vilivyowekwa na Marekani. Nchi nyengine ni Iran, Libya, Syria, Somalia, Yemen, Venezuela na Korea Kaskazini.
Katika taarifa yake, Rais Trump amesema nchi nyingine saba bado hazijaimarisha mifumo yao ya utoaji taarifa na zitasalia katika orodha hiyo. Wakosoaji wa Trump wamemtuhumu kwa kuweka vikwazo dhidi ya raia wa nchi nyengine kinyume cha katiba kwa kulenga nchi zilizo na idadi kubwa ya Waislam. Chad inachukuliwa kama rafiki wa Marekani katika mapambano dhidi ya ugaidi.